John David Washington, mtoto wa kwanza katika watoto 4 wa mkongwe wa filamu Hollywood Denzel Washington amekuwa nyota na kuweza kuonyesha zaidi ya kipaji katika series hiyo inayoendelea ijulikanayo kama “Ballers” ambayo imeingia season ya 2 July 2016.
J.D Washington mwenye umri wa miaka 32 ambae inasemekana amekimbia sana Hollywood sababu hakutaka atumike kuonekana kutokana na mafanikio ya baba yake ambae ni mshindi wa Academy Awards 2 hivi sasa.
J.D Washington akiwa na wazazi wake Denzel Washington na Mrs. Washington katika premier ya movie ya baba yake BOOK OF ELI
“I’ve had the acting bug since I was, like, five, But growing up I saw how people treated me differently when they knew who my father was, even the stuff I did on the field. Sometimes I’d rush for 100 yards and the headline would be, ‘Denzel’s son runs for 100 yards.’ That’s where the suppression of that bug came from.” JD Washington
JD Washington ambae aliamua kubobea kwenye mchezo ujulikanao kama American Football (NFL), pamoja na jitihada zake zilikuwa zikigonga ukuta mara kwa mara katika mchezo huo akiwa ameamua kupotezea kabisa kipaji cha usanii wa filamu sababu tu hakutaka achukuliwe au kupendelewa sababu ya baba yake na kutaka kutengeneza Empire yake mwenyewe.
Baada ya mambo ya NFL kutokwenda vizuri na kuumia katika moja ya mazoezi kiasi cha kukatishwa tamaa na makocha wake na pia yeye binafsi kuona NFL sio mahari pake tena. Wiki 3 baada ya kuumia mazoezini JD Washington alipata simu kutoka kwa agent wake kwenda kujaribu casting ya Ballers show ambayo inamshirikisha Dwayne “The Rock” Johnson. JD Washington aliingia katika usahili huo akiwa na magongo ya kutembelea akiwa bado kwenye matibabu baada ya kuumia na kufanikiwa kuipata nafasi hiyo baada ya kusailiwa mara 11.
JD Washington akiwa na The Rock kati ya schenes ndani ya Ballers
Pata nafasi ya kuweza kuangalia umahili wa msanii huyu katika series iitwayo “Ballers” ambayo kwa sasa ipo Season 2.
The post J.D Washington, mtoto wa Denzel Washington afanya kweli ndani ya “Ballers” appeared first on GongaMx.com.