Quantcast
Channel: Lifestyle – GongaMx.com
Viewing all articles
Browse latest Browse all 21

Professor Jay na Sholo Mwamba, Mmmhhhh!!!!! (VIDEO)

$
0
0

Enzi hizoo wakati harakati za muziki wa kizazi kipya ukiendelea nchini Tanzania kuna style nyingi sana zilianza kujitokeza kila msanii akitaka kuchukua nafasi yake katika fani ya muziki. Makundi pamoja na wasanii kutoka maeneo tofauti ya jiji la Dar Es Salaam yalianza kujitokeza kila mtu akiweka ubunifu wa aina ya juu kuweza kukubalika katika jamii, kati ya wachache ambao waliweza kupata attention yangu kutokana na utofauti wao wa Hip Hop ya kiswahili zaidi na wasanii wa makundi kama Waswahili waliopiga “Pengo” pamoja na Solid Groung Family waliojulikana sana kwa nyimbo yao “Bushi Party”.

Mtiririko au tunaweza tukasema mchakato mzima wa ukuwaji wa muziki wa kizazi kipya ukaja kudondokea kwenye mikono ya Profesor Jay baada ya muziki huu kukaa muda mrefu sana kutokuwa na muelekeo wa kukubalika katika lika zote mpaka hapo “Chemsha Bongo” ilipotoka na kuweza kukamata lika zote za Watanzania na kuweza kuelewa muziki wa kizazi kipya ni nini, kutokana na mistari na mashairi aliyoyapanga msanii huyu kuweza kuwaingia wananchi wa lika zote.

Muda si mrefu nimetoka kuangalia video ya KAZI KAZI, ngoma mpya ya Mheshimiwa Mbunge wa Mikumi Morogoro na Msanii Professor Jay ambae naweza kusema ni kati ya wasanii ambao wamekuwa wabishi sana kuweza kuamua kusimamia mchakato wa ukuaji wa muziki huu kwa miaka mingi sana mpaka sasa ameweza kubadilisha dhamila ya msanii kuwa mtu wa mtaani kuweza kuonyesha kuwa Msanii unaweza kuingia mpaka mjengoni (Bungeni) na ukabeba cheo cha Mheshimiwa na kufanya msanii kuweza kuheshimiwa.

KAZI KAZI ni ngoma ambayo naweza kusema umerudisha hadhi ya sanaa ambayo Professor Jay amekuwa akiibeba tokea hapo mwanzoni. Ujumbe ndani ya KAZI KAZI unaendana sana na dhamira safi ya Mhensimiwa mwenzake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli “Hapa Kazi Tu” ambayo imekuwa ikihamasisha sana wananchi kuzingatia na kuheshimu kazi kuweza kuleta maendeleo nchini.

Hapo mwanzo nimegusia nyimbo ya Solid Ground Family “Bushi Party” ambayo ilionyesha mazingira halisi ya Mtanzania wa hali ya chini akiwa anakura starehe katika party zao uswahili, nimeweza kuifananisha na video ya Kazi Kazi sababu maudhui yake yameendana, ila Kazi Kazi imefanyiwa kazi na ubunifu hali ya juu ambayo imeweza kumuonyesha ni jinsi gani Prof. Jay pamoja na mavazi aliyoyavaa ambayo ndio huvaliwa bungeni lakini ameweza kuendana (connect) vizuri sana na mazingira ambayo ni sawa na mazingira yake ya kazi kama mbunge, ambapo yeye binafsi ameweza kuyatofautisha mavazi pamoja na sehemu ya kazi.

Muonekano wa video tokea mwanzoni kuonyesha mazingira ya makazi kwa upande wa juu imeweza kutoa muongozo mzuri wa tegemezi la nini kinachoenda kutokea sababu wafanya kazi wengi nchini ni wenye maisha ya chini. Wavutaji, watumia madawa ya kulevya, wacheza kamali, wakabaji na wote ambao waliokuwa wanafanya maovu na kazi zisizo rasmi kuweza kuwaambia kuwa huu ni muda wa kufanya kazi ambapo mwishoni tunaona picha za watu wengi sana wakiendelea kufanya kazi.

Tukirudi kwa mtaalam mwenyewe Professor Jay, kitu ambacho nimependa zaidi pamoja na kuvaa suit lakini bado swagga za Hip Hop zimetembea vizuri sana akiwa kwenye stage, kiasi kwamba akaipoteza suit na kuonekana yeye zaidi. Ushirikisho wa Sholo Mwamba katika ngoma hii umeleta radha nzuri sana na kuifanya nyimbo kuwa tamu na kiswahili zaidi, vile vile wasanii wote wameweza kufanya style nzuri ambayo ni rahisi sana kuimba nao pamoja. Producer Mensen Selekta amefanya kazi nzuri sana kwenye beat, sababu hii beat inanikumbusha Hip Hop za uswahilini na imeendana sana na mazingira ya video na mashairi ya wasanii wote. Kwa kifupi yimbo ni nzuri sana na imebeba ujumbe mzito sana.

Hongera Professor Jay kuchaguliwa kuwa muwakilishi wa Mikumi na vile vile kwa kazi nzuri ya maana sana uliyoifanya kuhamasisha vijana kufanya Kazi.

Angalia Video hapa chini  “Kazi Kazi” Profesa Jay ft. Sholo Mwamba 

The post Professor Jay na Sholo Mwamba, Mmmhhhh!!!!! (VIDEO) appeared first on GongaMx.com.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 21

Trending Articles